Mwananchi wa kawaida wa Shaurimoyo, Zanzibar,hii ndio Mitaa yangu, nyumbani kwangu na ni sehemu ambapo Moyo wangu umependezwa napo.Unaweza kunitoa Nje ya Shaurimoyo ila hauwezi kuitoa Shaurimoyo ndani yangu.
"Nawakilisha Jimbo la Shaurimoyo kwa uadilifu na dhamira thabiti."
Katika kuendeleza Jimbo letu la Shaurimoyo na kuinua ustawi wa wananchi wake, tumeweka vipaumbele vifuatavyo
Elimu na Utawala wa Jimbo
• Kujenga Ofisi za Mbunge wa Jimbo la Shaurimoyo ili kutoa huduma za karibu kwa wananchi, kusikiliza kero zao,
na kuratibu utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa ufanisi zaidi.
• Kuboresha miundombinu ya shule zilizopo, ikiwemo madarasa, madawati, vyoo, maji safi, na mazingira bora ya kujifunzia.
• Kujenga madarasa mapya katika maeneo yenye msongamano wa wanafunzi.
• Kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya elimu bora bila ubaguzi.
• Kuhudumia makambi ya wanafunzi katika shule zote za jimbo kwa kuhakikisha yanakuwa na mazingira salama, chakula cha kutosha, na usimamizi bora.
• Kuwasaidia walimu wa madrasa zote kwa kuwatengea posho maalum ya kila mwezi kama utambuzi wa mchango wao katika malezi ya maadili ya watoto wetu.
• Kushirikiana na wazazi na viongozi wa jamii kuboresha elimu ya madrasa.
• Kusimamia udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi wote wanaopata nafasi za masomo kwa kushirikiana na Serikali. Wanafunzi wasiofanikiwa kupata udhamini rasmi watasaidiwa kupitia Mfuko Maalum wa Elimu wa Jimbo, utakaoundwa mahsusi kusaidia vijana wetu kufikia ndoto zao.
• Kuboresha vituo vya afya vilivyopo ili viweze kutoa huduma bora zikiwemo vipimo vya afya, dawa za kutosha, na watumishi wenye weledi.
• Kupatikana kwa magari ya wagonjwa (ambulance) katika kila kata ili kurahisisha huduma za dharura.
• Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu lishe bora, afya ya uzazi, usafi wa mazingira, na kinga dhidi ya magonjwa.
Kuchimba visima na kuimarisha miundombinu ya mabomba kwa usambazaji wa
maji safi na salama.
• Kusimamia miradi ya maji inayotekelezwa na serikali au wadau kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu.
• Kufanikisha kila shehia kuwa na upatikanaji wa maji safi kwa karibu kwa wananchi wote.
Kuwezesha vijana na wanawake kuunda vikundi vya ujasiriamali na kuunganishwa na mikopo nafuu kupitia halmashauri au taasisi za kifedha.
• Kutoa mafunzo ya stadi za
kazi, teknolojia na uendeshaji wa biashara kwa vijana ili kuongeza ajira na ubunifu.
• Kuweka mazingira bora ya uwekezaji wa biashara ndogo ndogo na viwanda vidogo ndani ya jimbo.
• Kutoa elimu rasmi kwa wajasiriamali wote wa Jimbo la Shaurimoyo, kulingana na kiwango na aina ya ujuzi wao, ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi, kuongeza kipato na kuchangia mapato ya jimbo.
• Kuboresha barabara za mitaa kwa kiwango cha changarawe au lami pale inapowezekana.
• Kujenga na kusafisha mitaro ya maji ya mvua ili kuzuia mafuriko na milipuko ya magonjwa.
• Kuweka taa za barabarani katika maeneo ya makazi ili kuongeza usalama wa wananchi hasa nyakati za usiku.
Kujenga mshikamano baina ya wananchi wa itikadi mbalimbali kwa msingi wa heshima, haki na
na usawa.
• Kuhimiza ushirikiano kati ya viongozi na wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo ya jimbo.
• Kupinga ubaguzi, siasa za vitisho na migawanyiko kwa lengo la kulinda umoja, amani na mshikamano wa Shaurimoyo.
Nimezaliwa na kukulia Shaurimoyo, nikasoma shule za
hapa, na nimejitoa kwa moyo wote kuwatumikia wananchi. Safari yangu ya kazi imepita kwenye
benki, bima, usafirishaji, na uongozi wa michezo.
Nawakilisha Jimbo la Shaurimoyo kwa uadilifu na dhamira thabiti.
"
Naamini kwa kushirikiana na wananchi wote wa Jimbo la Shaurimoyo, tutaleta mabadiliko ya kweli.
Hii ni safari ya matumaini, mshikamano, na maendeleo ya wote.
⸻
#ShaurimoyoKwanza
#MaendeleoKwaVitendo
#KaziNaUwazi